Wednesday, April 17, 2013

UKRISTO NA DHIKI

mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.
 [1 Wathesalonike 3:3]



Katika maeneo magumu sana kwa mkristo anayesafiri ni kukubaliana asilimia mia moja na ukweli halisi wa kimungu kuhusu taabu, shida na dhiki.

Biblia inashangaza pia hata katika waraka wa Yakobo pale unapohimiza watu kuhesabu kuwa ni furaha tupu tunapopita katika majaribu mbalimbali.

Dhiki haipendezi. Dhiki ni ngumu kukubaliana nayo. Baadhi ya mambo nyeti kama kifo yamefichwa kwetu na Mungu. Mungu anajua kwamba kwa akili zetu za kibinadamu hatupendi shida au mateso. Mungu angeweza kuruhusu kwa mamlaka tuliyopewa kwamba, ukiona kuna jaribu wiki kesho basi unaumba kifo wiki hii na unaondoka duniani ili wiki kesho usipate jaribu fulani.

Hata na wale wenye pesa nyingi hawana uwezo wa kukwepa matatizo na dhiki zote. Katika dhiki tunatakiwa kujinyenyekeza kwa Mungu wetu.

Mungu anataka tupitie kwenye dhiki. Tuahitaji kumuomba yeye atuwezeshe kuhesabu kuwa ni furaha tupu kuingia katika majaribu mbalimbali.

Monday, April 15, 2013

FURAHA YA SIKU ZOTE



Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. (Wafilipi 4:4)

Ni jambo la ajabu sana kwamba biblia inatutaka tufurahi kila siku, kila saa, kila wiki, kila mwezi, kila dakika. Biblia ni kitabu cha ajabu sana. unaweza kujiuliza swali kwamba je, haioni kwamba wakati mwingine tunakuwa tumehuzunishwa na huzuni ya mambo kadha wa kadha. Siku zote haijaweka siku za kuruka.

Ndani ya siku zote kuna wakati ambapo mtu amefiwa. Msiba ni jambo ambalo kibinadamu linasikitisha. Neno linataka ufurahi, nifurahi siku zote. Ukiwa unadaiwa deni si wakati mzuri. Neno linataka wenye madeni wafurahi siku zote. Ukiwa kwenye foleni ya kuchapwa viboko shuleni si wakati mzuri. Wewe mwanafunzi biblia inakutaka ufurahi siku zote ikiwa ni pamoja na wakatiunasubiri kupigwa.



Umeomba mke au mume kutoka kwa Bwana, na bado hujaona matokeo katika macho ya nyama, bado neno halisemi ulalamikelalamike kwa watu. Unayesubiri mwenzi wa ndoa inapasa ufurahi katika Bwana siku zote.

Nini cha kuto kukufanya ufurahi siku zote katika Bwana? Je ni njaa, au deni, au kukosa nguo, au kuishiwa, au kuumwa, au kukimbiwa na mume/mke, au watoto kuwa wakorofi sana, orodha ni ndefu. 

Ukamilifu wa Mungu kwa mtu aliyeokoka unajikita katika ujumbe maalum wa kufurahi siku zote