Wednesday, February 25, 2015

CHANZO CHA MAARIFA


Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. [Mithali 1:7]

Tunaishi katika nyakati ambazo kuishi kipagani ni namna inayoabudiwa na kutukuzwa kila kona ya dunia. Matendo ya watu kadha wa kadha yanaonyesha jinsi ambavyo tuna kazi kubwa ambayo hatujaifanya.

Ukienda mjini utasikia matusi makubwa yakitoka katika vinywa vya watu. Mungu hakuumba kinywa ili kitumike vyovyote tu. Mungu anataka mie nawe tumtukuze Mungu kwa midomo yetu.

Mtu akisoma sana anaonekana kama ana maarifa mengi na anaopata sifa nzuri katika jamii. Mtu akiwa na ufahamu mkubwa wa biblia haonekani kuwa wa maana. Hii yote ni kazi ya yule mwovu ibilisi.

Mwenye elimu haswa ni yule amchaye Bwana.

Maarifa ya kweli ni kumcha Mungu na kuzifuata njia zake.