Monday, April 15, 2013

FURAHA YA SIKU ZOTEFurahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. (Wafilipi 4:4)

Ni jambo la ajabu sana kwamba biblia inatutaka tufurahi kila siku, kila saa, kila wiki, kila mwezi, kila dakika. Biblia ni kitabu cha ajabu sana. unaweza kujiuliza swali kwamba je, haioni kwamba wakati mwingine tunakuwa tumehuzunishwa na huzuni ya mambo kadha wa kadha. Siku zote haijaweka siku za kuruka.

Ndani ya siku zote kuna wakati ambapo mtu amefiwa. Msiba ni jambo ambalo kibinadamu linasikitisha. Neno linataka ufurahi, nifurahi siku zote. Ukiwa unadaiwa deni si wakati mzuri. Neno linataka wenye madeni wafurahi siku zote. Ukiwa kwenye foleni ya kuchapwa viboko shuleni si wakati mzuri. Wewe mwanafunzi biblia inakutaka ufurahi siku zote ikiwa ni pamoja na wakatiunasubiri kupigwa.Umeomba mke au mume kutoka kwa Bwana, na bado hujaona matokeo katika macho ya nyama, bado neno halisemi ulalamikelalamike kwa watu. Unayesubiri mwenzi wa ndoa inapasa ufurahi katika Bwana siku zote.

Nini cha kuto kukufanya ufurahi siku zote katika Bwana? Je ni njaa, au deni, au kukosa nguo, au kuishiwa, au kuumwa, au kukimbiwa na mume/mke, au watoto kuwa wakorofi sana, orodha ni ndefu. 

Ukamilifu wa Mungu kwa mtu aliyeokoka unajikita katika ujumbe maalum wa kufurahi siku zote

No comments:

Post a Comment