Tuesday, December 18, 2012

UMUHIMU WA UDONGO MZURI8 Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia."  (Luka 4:8)


Tunahitaji kuzaa matunda yanayokaa. Katika hali ya kawaida bila udongo mzuri mazao hayatastawi kabisa. Pasipo udongo mzuri kukua ni ndoto za abunuasi. Pasipo udongo mzuri tusitegemee nguvu za Mungu. Pasipo udongo mzuri tusitegemee kujitoa kikamilifu kwa Yesu. Pasipo udongo mzuri hakuna kujaa na kufurika. Pasipo udongo mzuri tusitegemee uamsho kwa mtu au kwa kundi. Udongo upo wa aina nyingi. Hata wakulima wanapotaka kupanda mazao yao hawaendi popote tu wakapanda mbegu. Mkulima mzuri atachagua mahali panapofaa kwa mbegu zake kuota na kukua.


Je mimi na wewe tupo katika udongo gani? Je ni mfinyanzi? Je, ni mchanga, Je, ni udongo mzuri?


Maadamu mbegu ni mfano wa mtu, hakuna bahati mbaya katika kupandwa kwenye udongo usiofaa. Mtu mwenyewe anajipeleka kwenye udongo mzuri au ule usiofaa. Uchaguzi wa wapi ukapandwe kama mkristo ni wako wewe mwenyewe.


Ukitaka kukua na kuongezeka au kuzaa unajikita kwenye udongo mzuri. Ukitaka kuwa mkristo wa kawaida bila kuwa na matunda unajikita kwenye mwamba, kwenye miiba au popote pasipokuwezesha kukua na kuongezeka. Hii ni mada endelevu.


Barikiwa

No comments:

Post a Comment