Bwana atainyosha
toka sayuni
Fimbo ya nguvu
zakoUwe na enzi kati ya adui zako. (zaburi 110:2)
Tunapoendelea kuishi katika maisha ya wokovu au utauwa,
tunakutana na vikwazo, milima, visiki, mawe, magonjwa, njaa, kuishiwa, madeni,
kuchukiwa, kuonewa, upinzani, kukosa uhuru na mengine mengi. Tunakutana na hayo
kwa sababu hayo ni sahemu ya dunia tunayoishi. Hatupandishwi daraja bila
kushinda katika hayo. Mwimba zaburi anaposema adui, analenga vitu vyote nilivyotaja hapo juu. Mengine
yameendelea kuwa changamoto kwetu hata wakati ambao tumeyakemea au kuomba
yaondoke kabisa.
Pamoja na changamoto za namna moja au nyingine, neno la Mungu
linatukumbusha kwamba tunayo fimbo. Hii ni alama ya mamlaka. Fimbo yako ni
mamlaka yako. Ahadi imetolewa. Kama ukishaielewa ni ahadi ya jinsi gani na
uidai vipi kwa Bwana basi utachangamka. Wewe dai ahadi ya fimbo yenye nguvu.
Fimbo hii itanyoshwa kutoka sayuni, na siyo kutoka Mabwepande
au Makambako. Fimbo hii haitanyoshwa kama kubofya rimoti ya TV. Fimbo hii
inatafutwa. Fimbo hii inahangaikiwa. Tunajua sana kwamba hata Yesu mwenyewe
alisema kwamba ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu. Fimbo inanyoshwa kutoka
Sayuni. Sayuni ni kwenye maombi. Sayuni ni kwenye ibada. Sayuni ni kwenye sifa.
Sayuni ni kwenye maombi ya kujitoa. Sayuni ni kwenye kusoma neno.Sayuni ni
katika kutafakari neno na kupata mafunuo.
Vitu nilivyovitaja hapo juu vinashindika tu mbele za Mungu kupitia
Mfalme Yesu. Ni hiyo fimbo yenye nguvu inayoleta jibu kwako.
Tafakari
No comments:
Post a Comment